UTANGULIZI
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ina Jukumu la kusimamia na kuratibu utoaji wa Elimu nchini kwa kuandaa Sera, Sheria na Miongozo mbalimbali kutoka ngazi ya Elimu ya Awali hadi Elimu ya Juu. Aidha, Wizara ina jukumu la kusimamia na kuratibu maendeleo ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu; pamoja na matumizi yake katika nyanja mbalimbali ikiwemo Biashara, Viwanda, Kilimo na Maisha ya kila siku kwa ujumla.
Kwa mujibu wa Hati idhini iliyotolewa tarehe 22 Aprili 2016, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknoloji inatekeleza majukumu yafuatayo:
Kutunga na kutekeleza Sera za Elimu, Sayansi, Utafiti, Huduma za Maktaba, Sayansi, Teknolojia, Ubunifu na Uendelezaji wa Mafunzo ya Ufundi;
Kuendeleza Elimumsingi kwa kutoa Ithibati ya Mafunzo ya Ualimu na Maendeleo ya kitaalamu ya Walimu;
Kubainisha Vipaji na kuviendeleza;
Kusimamia Uendelezaji wa Mafunzo katika Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi;
Kusimamia Mfumo wa Tuzo wa Taifa;
Kuainisha Mahitaji ya Nchi katika Ujuzi na Kuuendeleza;
Kuweka Viwango vya Taaluma ya Ualimu;
Kusimamia Ithibati na Uthibiti wa Shule;
Kusimamia Huduma za Machapisho ya kielimu;
Kutegemeza/Kuimarisha Utumiaji wa Sayansi, Uhandisi, Teknolojia na Hisabati;
Kuendeleza Wataalamu wa ndani katika Sayansi, Teknolojia na Ubunifu:
Utafiti katika Sayansi na Teknolojia;
Uendelezaji wa Rasilimaliwatu na Uongezaji Tija ya Watumishi walio chini ya Wizara; na
Kuratibu Shughuli za Idara, Mashirika, Wakala, Programu na Miradi iliyo chini ya Wizara.
MALENGO YA WIZARA
Ili kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imejiwekea malengo yafuatayo:
Kuongeza Fursa na Ubora wa Elimu na mafunzo katika ngazi zote;
Kutunga na kutekeleza Sera za Elimu, Utafiti, Huduma za Maktaba, Sayansi, Teknolojia, Ubunifu na Uendelezaji wa Mafunzo ya Ufundi
Kuimarisha Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa katika Elimu, Sayansi na Teknolojia;
Kuratibu na kuimarisha maendeleo ya Utafiti na Ubunifu kwa ajili ya Kukuza Uchumi wa Jamii na Maendeleo ya Viwanda;
Kuongeza matumizi na mafunzo pamoja na kuweka kanuni za kuwezesha matumizi salama ya Teknolojia na Nyuklia;
Kukusanya rasilimali fedha na kuongeza uwekezaji katika Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ubunifu pamoja na miundombinu;
Kuimarisha masuala ya Menejimenti ya Habari katika Sekta ya Elimu pamoja na Ujifunzaji wa Kielektroniki (E-learning);
Kuimarisha mazingira ya kazi ili kuongeza tija na ufanisi katika utoaji wa huduma; na
Kushughulikia Masuala Mtambuka katika Sekta ya Elimu.