UKARIBISHO WA BONDE

Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu ina jukumu la kulinda, kutunza na kuhifadhi Rasilimali za maji na Mazingira kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji Namba 11 ya Mwaka 2009. Katika kutekeleza sheria hii ya kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji.

Bodi ya maji bonde la wami/ruvu inawakaribisha wadau, wajumbe na watumiaji wote wa maji katika Tovuti yetu kwa huduma mbalimbali pamoja na maoni ya utendaji kazi. Kumbuka Kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji ni jukumu letu sote, hivyo basi tulinde na kuhifadhi vyanzo vya maji kwa maendeleo ya taifa letu.